Service Worker ndiyo inafanya website yako kuwa App-ish, ikiwa na uwezo wa:


Kufanya offline browsing


Kuwa na caching


Speed ya juu


β€œAdd to Home Screen”


Kuongezeka performance ndani ya app


Mfano wetu: Faulink.com (Website tayari imetengenezwa vizuri na responsive design).

πŸ“Œ Description
Katika hatua hii utafundishwa:


Kazi ya Service Worker


Kuunda service-worker.js file


Kuunganisha website na Service Worker


Kuweka caching ili app ifunguke bila intaneti


Kutengeneza folder structure ya PWA


Baada ya hatua hii, website yako itakuwa tayari ku-convert kuwa real Android App kwa hatua inayofuata.

πŸ›  1. Unda Faili Linaloitwa service-worker.js
Hili ni faili muhimu sana. Liweke kwenye root directory ya website.
✳ service-worker.js
const cacheName = "faulink-cache-v1";
const filesToCache = [
"/",
"/index.php",
"/manifest.json",
"/icons/icon-192.png",
"/icons/icon-512.png"
];

self.addEventListener("install", event => {
event.waitUntil(
caches.open(cacheName).then(cache => {
return cache.addAll(filesToCache);
})
);
});

self.addEventListener("fetch", event => {
event.respondWith(
caches.match(event.request).then(response => {
return response || fetch(event.request);
})
);
});

βœ” Hii inasaidia website kufanya kazi hata kama network ni ndogo.
βœ” App itakuwa inapakia haraka sana.

πŸ›  2. Link Service Worker Kwenye HTML
Weka script hii kwenye footer ya website yako (kabla ya </body>):
<script>
if ("serviceWorker" in navigator) {
navigator.serviceWorker.register("/service-worker.js")
.then(() => console.log("Service Worker Registered"));
}
</script>


πŸ›  3. Hakikisha Manifest Inaungana na Service Worker
Kwa nini?
Kwa sababu manifest ndiyo inasema:


App name


Icon


Theme color


Display mode (standalone)


Mfano wa manifest yako:
{
"name": "Faulink App",
"short_name": "Faulink",
"display": "standalone",
"start_url": "/",
"background_color": "#ffffff",
"theme_color": "#0d6efd",
"icons": [
{
"src": "/icons/icon-192.png",
"sizes": "192x192",
"type": "image/png"
},
{
"src": "/icons/icon-512.png",
"sizes": "512x512",
"type": "image/png"
}
]
}


πŸ“± 4. Jaribu Kama PWA Imefanya Kazi
βœ” Chrome Steps:


Fungua website yako


Nenda Inspect β†’ Application


Cheki:


Manifest: βœ”


Service Worker: βœ”


Cache Storage: βœ”




βœ” Simu (Android Chrome):


Tembelea website


Gusa dot 3


Chagua Add to Home Screen


Ikiwa unapata Install App, basi PWA yako imefanikiwa πŸŽ‰

πŸ§ͺ 5. Test Offline Mode
Zima data/wifi β†’ Fungua website
Ikiwa inafunguka basi service worker yako imefanikiwa kufanya cache.
Mfano: Faulink.com unaweza kuifanya ifanye offline caching ya sehemu muhimu za system.

πŸ”š Hitimisho la Hatua ya 3
Hatua hii imekamilisha sehemu muhimu ya kufanya website yako kuwa:


Offline-ready


Faster


Installable


PWA-ready


Sasa website yako iko tayari kuanza hatua inayofuata:
πŸ‘‰ Kubadilisha kuwa Real Android APK β€” Free Tools

πŸ”— Links Za Kujifunza Zaidi
🌐 Faulink Official Website:
https://www.faulink.com/
πŸ“˜ Jifunze Web Design & Programming:
https://www.faulink.com/excel_mifumo.php
πŸ“² Piga / WhatsApp kwa msaada wa haraka:
https://wa.me/255693118509